Wanariadha 64 Kenya kuwakilisha mbio za Shirikisho Afrika

Nairobi. Timu ya wanariadha 61, wakiongozwa na bingwa wa dunia wa zamani wa dunia wa kurusha mkuki, Julius Yego, mkali wa kuruka viunzi, Conseslus Kipruto na bingwa wa mbio za mita 5000, Bernard Manangoi, wanaondoka nchini kesho kuelekea Nigeria kwa ajili ya kushiriki makala ya 21 ya mbio za Shirikisho Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la Riadha nchini (AK), wanariadha hao wataondoka nchini kuelekea Assaba Nigeria, wakitumia ndege ya shirika la ndege la Kenya, KQ 532, majira ya saa 2.10 asubuhi, kesho Jumatatu, Julai 30, ambako watashiriki makala ya 21 ya mbio hizo, zitakazofanyika Agosti 1-5.
Mbali na Manangoi, Kipruto na Yego, bingwa wa Dunia, mita 5000 wanawake,  Champion Helen Obiri naye ataondoka na kikosi hicho. Wanariadha wengine ni Bingwa wa zamani wa Dunia, mita 400 kuruka viunzi, Nicholas Bett, mshindi wa medali ya shaba wa michezo ya Olimpiki, mita 800, Margaret Nyairera, ingizo Eunice Sum na Pauline Korikwang.
Katika kikosi hicho, Kenya itawategemea wanariadha wengine kama Alice Aprot (mita 10,000), William Sawe (kuruka juu), Samuel Gathimba (Kilomita 20 kutembea) na Grace Wanjiru (Kilomita 20, kutembea), katika harakati za kusaka ubingwa huko Nigeria.
Aidha, matumaini ya Kenya, katika kuendeleza rekodi nzuri walioiweka katika makala ya 20 ya mbio hizi, huko Durban Afrika Kusini, yatahitaji ushiriki mzuri wa ingizo jipya kadhaa wakiongozwa na Celliphine Chespol (mita 3,000, kuruka viunzi na maji).
Emmanuel Korir, anayeishi Marekani (mita 400), kinda wa miaka 17, Samuel Chebulei (mita 5,000) na bingwa wa Dunia wa vijana (2016), kuruka viunzi na maji, Amos Kirui. Katika makala ya 20, Kenya ilimaliza wa pili, nyuma ya Wenyeji Afrika Kusini, wakiwa na medali 24 ( dhahabu 8, fedha 8 na shaba 8).