Natasha, Mzee Chilo, Gabo watikisa jukwaa ZIFF

Wednesday July 11 2018

 

By Rhobi Chacha

Zanzibar. Wasanii wa filamu za kibongo Natasha,Mzee Chilo,Gabo usiku wa kuamkia leo wamefurahisha watu waliohudhuria kwenye tamasha la ZIFF 2018,walipocheza kwa kukata mauno baada ya igizo la jukwaani kumalizika katika Tamasha la Ziff 2018,viwanja vya Ngome Kongwe.
Tamasha hilo lililohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo  kutoka hapa nchini na nje ya nchi, walikuwa makini kuangalia igizo la  'Mrs Lucy Goes to Africa' lililokuwa limejaa vichekesho vya kutosha.
Tamasha hili la ZIFF litaendelea mpaka Julai 15 huku kila siku filamu mbalimbali zikionyeshwa kwenye kumbi za hoteli zinazozunguka mji Mkongwe , sambamba na semina za mafunzo ya uandaaji na uongozaji wa filamu yatakayotolewa na waongozaji wakubwa kutoka nchi mbalimbali.
Hata hivyo waandaaji wa tamasha hilo wamesikitishwa na mwamko mdogo wa wasanii wa filamu za kibongo katika tamasha hilo.

Advertisement