Salamba hatihati nusu fainali Kagame

Monday July 9 2018

 

By THOBIAS SEBASTIAN

STRAIKA wa Simba, Adam Salamba ambaye amefunga mabao matatu katika mashindano ya Kombe la Kagame huenda akaikosa nusu fainali ya mashindano hayo.

Salamba aliumia katika mechi ya nusu fainali baada ya kuchezewa faulo na mabeki wa As Sport ambayo ilipekea kuchanika nyama za paja za mguu wa kushoto.

Wakati timu ya Simba wakiondoka uwanjani hapa baada ya mechi kumalizika Salamba alikuwa akichechemea na kushikiliwa yaani kupewa msahada wa kutembea kwani alikuwa hawezi kutembea pekee yake.

"Nimechanika nyama za paja na nipo hospitali naendelea na matibabu bado sijapata ruhusa kwamba naweza kucheza mechi ya nusu fainali au sitacheza,"

"Mimi mwenyewe hali ya mguu wangu naiona bado haijakaa sawa kwani bado nasikia maumivu hata kutembea napata shida," alisema Salamba ambaye yupo katika vinara wanaongoza kufunga kwenye mashindano hayo.

Advertisement