Yanga, Simba zaigeuza Mtibwa Sugar shamba la bibi

Monday July 9 2018

 

By OLIPA ASSA

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kitu kikubwa anachokifanya kwa wachezaji wake ni kubadili mitazamo yao na kujiona wa kimataifa huku akisema wanapaswa kuongeza bidii ndio maana Simba na Yanga zinachukua wachezaji wake.

Ametoa kauli hiyo kufuatia majukumu yaliopo mbele yao ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa FA kwa kuwafunga Singida United kwenye fainali hizo.

"Nimegundua kuna kitu kinakuwa kinajengeka kwa wachezaji kuwaona wa kimataifa ni wale ambao wanachezaji michuano ya Klabu Bingwa na Shirikisho na ndio maana naamua kuwaweka kwenye mtazamo huo.

"Kikubwa nawaambia namna wanavyoweza wakafanya maajabu kwenye michuano hiyo, kuliko wanavyodhania na nawasisitiza na ndio maana klabu za Simba na Yanga zilizozoeleka kushiriki, zinachukua wachezaji Mtibwa Sugar na wanakuwa tegemeo ndani ya vikosi vyao,"anasema.

 

Advertisement