Chilunda ala kiapo Azam

Sunday June 10 2018

 

By OLIPA ASSA

STRAIKA wa Azam FC, Shaaban Idd Chilunda amesema tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa Mei imempa mzuka wa kumfanya aongeza nguvu ili msimu ujao atishe zaidi.

Chilunda aliibuka mshindi wa tuzo hiyo akiwazidi ujanja Jacob Massawe wa Ndanda na Edward Christopher wa Kagera Sugar na alisema anashukuru kwa heshima aliyopewa, pia ni changamoto ya kuhakikisha msimu ujao anakuwa mkali zaidi.

“Kitendo cha kuwa Mchezaji Bora wa Mei si jambo dogo kwangu, linanipa nguvu ya kuongeza juhudi zaidi na kuona nina uwezo wa kufanya vitu vikubwa.

Naye Jacob Massawe alimpongeza Chilunda aliyeifungia Azam mabao tisa ya Ligi Kuu kwa kuibuka kidedea mbele yao akimtaka asivimbe kichwa.

“Nampongeza Chilunda ni mchezaji mzuri, kikubwa aendeleze juhudi zake ili msimu unaokuja kipaji chake kizidi kunawiri kwa lengo la kufanyika msaada kwa klabu yake na timu ya Taifa Stars,” alisema.

Advertisement