Yanga yatua salama Ethiopia

Sunday April 15 2018

 

By Khatimu Naheka

Addis Ababa.Baada ya safari ya saa tisa,Yanga imetuma salama Addis Ababa, Ethiopia na kuanza safari ya basi kuelekea Awassa kuwafuata Wolaitta Dicha.

Yanga ipo Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya mashindano.

Katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda wa mabao 2-0 dhidi Wolaitta Dicha hivyo mabingwa hao wanahitaji sare yoyote ili kusonga mbele.

Safari ilivyokuwa

Mpaka inafika jijini Awassa Yanga ilitumia saa tisa njiani ambapo kati ya hayo manne pekee ndiyo yaliyotumika angani wakitumia saa mbili kutoka jijini Dar es Salaam kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya.

Kutoka hapo ilitumia saa nyngine mawili ikitua Uwanja wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa nchini Ethiopia safari hiyo wakitumia ndege ya Shirika la Kenya.