Hazard, De Bruyne waibeba England

Madrid, Hispania. Wachezaji wa Real Madrid wametawala katika kikosi cha nyota bora 11 kwa mwaka 2017, wakati Ligi Kuu England ikiingiza wachezaji wawili tu.

Kikosi hicho cha wachezaji bora wa mwaka ni kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wasomaji wa Mtandao wa UEFA.com kuanzia Novemba 22,2017 hadi Januari 10, 2018.

Mashabuiki wa soka walitakiwa kuchagua wachezaji bora Xl katika orodha ya wachezaji 50 waliotajwa na katika tovuti ya UEFA.com  ( makipa 5, mabeki 15, viungo 15 na washambuliaji 15).

Nyota wa Real Madrid walioingia katika kikosi hicho ni Sergio Ramos, Marcelo, Kroos, Modric na Cristiano Ronaldo wakati Lionel Messi akiwa ni mchezaji pekee wa Barcelona.

Kutoka katika Ligi Kuu England wameingia De Bruyne (City) na Hazard (Chelsea), huku Buffon na Chiellini (Juventus) wakibeba Serie A na beki Dani Alaves (PSG) akiwakilisha Ligue 1.

Hivi hapa chini ni vikosi bora kwa miaka mitano iliyopita.

2016: Buffon; Boateng, Pique, Ramos, Bonucci; Modri, Kroos, Iniesta; Messi, Griezmann, Ronaldo.

2015: Neuer; Alves, Pique, Ramos, Alaba; Pogba, Iniesta, James; Messi, Neymar, Ronaldo.

2014: Neuer; Lahm, Godín, Ramos, Alaba; Kroos, Robben, Di Maria; Messi, Ibra, Ronaldo.

2013: Neuer; Lahm, Thiago Silva, Ramos, Alaba; Bale, Reus, Ozil, Ribery; Ibra, Ronaldo.

2012: Casillas; Ramos, Pique, Thiago Silva, Lahm; Iniesta, Xavi, Pirlo, Ozil; Messi, Ronaldo.