Mashabiki wamuondoa Ommy Dimpoz kuimba, wampeleka uanamitindo

Thursday January 11 2018

 

By RHOBI CHACHA

Mwanamuziki Ommy Dimpoz ameshauriwa na mashabiki wake kuwa ajihusishe na mambo ya mitindo sio muziki peke yake.

Mashabiki hao wamedai kuwa, Ommy Dimpozi kutokana na kujua kujipangilia kimavazi, nywele na mapozi akiwa anapiga picha, basi itapendeza zaidi akiwa mwanamitindo.

 

Hata hivyo shabiki wake mwingine alidai kuwa, Dimpoz akiwa mwanamitindo atapiga pesa sana kutokana na kuwa na sifa ya uanamitindo.

"Mie sisemi kuwa aache muziki hapana,ila akili yake angeipa asilimia kubwa kwenye uanamitindo na ubunifu wa mavazi kwa ana sifa zote na angepiga pesa balaa" alisema mmoja wa shabiki wake, Fadhili.