Takukuru kukamilisha uchunguzi kesi Malinzi

Dar Es Salaam. Kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili, imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi hiyo limepelekwa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa( Takukuru) kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

Malinzi na aliyekuwa Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga wanakabiliwa na mashtaka 28, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Takukuru, Leornad Swai aliieleza hayo leo mahakama hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa jalada la kesi hiyo limeshatoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu(DPP) na sasa limepelekwa Takukuru kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

"Jalada la kesi hii limeshatoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu (DPP) na sasa limepelekwa Takukuru kwa ajili ya kurekebisha vitu vichache na  kukamilisha uchunguzi, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa" alidia Swai

Baada maelezo hayo, wakili wa Utetezi, Nehemia Nkonko aliomba upelelezi wa shauri hilo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi kwa haraka na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 25, itakapotajwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha Dola za Marekani, 375,418.
Washtakiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 

Katika kesi hiyo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 na katika shtaka la kwanza kwani Malinzi na Mwesigwa  Juni 5,2016 Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya walighushi nyaraka zinazoitwa “Executive Committee Resolution” za Juni 5,2016 wakionesha kamati tendaji ya TFF imebadili mtia saini wa akaunti ya benki ya TFF kutoka kwa Edgar Leonard Masoud kwenda kwa Nsiande Isawafo Mwanga wakati wakijua si kweli.

Katika shtaka la pili,inadaiwa kuwa Septemba Mosi, 2016 katika benki ya Stanbic tawi la Kinondoni, Mwesigwa aliwasilisha nyaraka ya kughushi.

Katika shtaka la tatu, inadaiwa kuwa Desemba 17,2013 huko TFF, Jamal Malinzi alighushi risiti namba 308 ya Novemba 6,2013 akionesha ameikopesha TFF  dola za Kimarekani 9,300 (Sh 19milioni), wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la nne, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi hiyo ya TFF, alighushi risiti namba 322 ya Desemba 17, 2013 akionyesha ameikopesha TFF dola za Marekani 10,000(Sh20milioni) wakati si kweli.

Pia, shtaka la tano, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17, 2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 323 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD 18,000(sh37milioni).

Iliendela kudai kuwa ,katika shtaka la sita kuwa  Desemba 17,2013, Malinzi kwenye ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 324 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD 500(Sh10 milioni).

Katika shtaka la saba, Malinzi anadaiwa kuwa Desemba 17,2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 325 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD 1,032(Sh 2milioni) wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la nane kuwa  Machi 26,2014  katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1956 ya Machi 26,2014 akionesha ameikopesha TFF dola za Kimarekani 40,000(Sh 84milioni) wakati akijua si kweli.

Inadaiwa katika shtaka la tisa kuwa Machi 13,2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1957 ya Machi 13,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 5000(Sh 10milioni).

Aliendelea kudai kuwa katika shtaka la kumi, kuwa Mei 13, 2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1624 ya Mei 13,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 40,000(sh84milioni).

Katika shtaka la 11, Katuga alidai kuwa Mei 16, 2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1634 ya Mei 16, 2014 akionesha ameikopesha TFF USD 10,000(sh20 milioni).

Shtaka la 12, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 11,2014 katika ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 1860 ya Julai 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 15,000(Sh30milioni).

Kwa upande wa shtaka la 13, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 11, 2014 katika ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 1861 ya Julai 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 3,000(Sh 6milioni).

Inadaiwa katika shtaka la 14, kuwa Julai 15,2014 katika ofisi hiyo ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1863 ya Julai 15,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 14,000( Sh 28milioni).

Iliendelea kudaiwa katika shtaka la 15, kuwa Julai 15,2014, Malinzi katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 1866 ya Julai 15,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 4000(Sh 8 milioni).

Shtaka la 16, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 25,2014  kwenye ofisi ya TFF  alighushi risiti namba 1876 ya Julai 25, 2014 akionesha TFF imeikopesha TFF USD 1,000(Sh 2milioni).

Kwa upande wa shtaka la 17 inadai kuwa Agosti 19,2014 huko TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1890 ya Agosti 19,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 5000(Sh 10 milioni).

Kwenye shtaka la 18, Katuga alidai kuwa Oktoba 11,2014 kwenye ofisi hizo za TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1568 ya Oktoba 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 1,200 (2.4milioni) wakati akijua sikweli.

Shtaka la 19, Malinzi anadaiwa kuwa Agosti 17,2015 kwenye ofisi hiyo ya TFF  alikula njama ya kughushi risiti namba 1511 ya Agosti 17,2015 akionesha ameikopesha TFF USD  5,000(Sh 10milioni).

Shtaka la 20, alidai kuwa Julai 22,2015 kwenye ofisi za TFF, Malinzi alighushi risiti namba 2981 ya Julai 22,2015 akionesha ameikopesha TFF USD 2,000(Sh 4milioni).

Shtaka la 21 alidai kuwa Mei 9,2016 kwenye ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 832 ya Mei 9,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 7000(Sh14milioni) wakati akijua si kweli.

Shtaka la 22, inadaiwa kuwa, Juni 16,2016 katika ofisi ya TFF iliyopo Ilala Dar es Salaam, Malinzi alighushi risiti namba 931 ya Juni 16,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 10,000(Sh20 milioni).

Inadaiwa katika shtaka la 23, kuwa Malinzi Agosti 2, 2016 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namb 947 ya Agosti 2,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 1,000(Sh 2milioni).

Akiendelea kusoma hati, alidai katika shtaka la 24 kuwa Septemba 19,2016 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1029 ya Septemba 19,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 1,000(Sh 2milioni).

Katika shtaka la 25, anadai kuwa Septemba 22,2016 katika ofisi ya TFF, Malinzi alikula njama ya kughushi risiti namba 1071 ya Septemba 22,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 15,000(Sh30milioni).

Kwenye shtaka la 26 ilidaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,2016 washtakiwa Malinzi, Mwesigwa na Nsiande kwa pamoja na kwa kushirikiana walitakatisha fedha kiasi cha USD 375,418 huku wakijua fedha hizo ni zao la kughushi.

Katika  shtaka la 27, Malinzi na Mwesigwa wanadaiwa kuwa  katika kipindi hicho cha Septemba Mosi na Oktoba 19,2016 katika benki ya Stanbic  tawi la kati la Kinondoni  walijipatia USD 375,418 wakati wakijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la 28, Mwanga anadaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,2016 katika ofisi ya TFF alimsaidia Malinzi na Mwesigwa kujipatia USD 375,418 kutoka banki ya Stanbic huku akijua upatikanaji wake umetokana na kughushi.