Zahera anataka mabao tu Yanga

Muktasari:

 Katika mazoezi yanayoendelea hivi sasa ya Yanga, sio beki wala kiungo, Nyota wote wamekomaliwa kufunga.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameendelea kukinoa kikosi chake ambapo mazoezi ya leo yamefanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa lakini katika mazoezi yake amekomalia sana zoezi la kufunga kuliko kuzuia.
Katika mazoezi yanayoendelea hivi sasa wachezaji wote wa Yanga wanafundishwa mbinu za kufunga ambapo straika mpya David Molinga ameonekana kuliwezea zaidi zoezi hilo kwani amekwamisha mipira mingi wavuni kuliko wengine.
Katika zoezi hilo, mshambuliaji Juma Balinya aliyeivusha Yanga hatua inayofuata kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Township Rollers ameonekana kutokuwa fiti kwani mguu wake wa kulia haupo fiti na hivyo anatumia zaidi mguu wa kushoto.
Kwenye maelekezo ya Zahera amekuwa akiwasisitiza sana kuongeza spidi pindi walionapo lango na zoezi hilo limekua rahisi kwa Mrisho Ngassa na Sedney Urkhob ambao wameonyesha kuwa na mbio zaidi