Yanga Princess yaiharibia Tanzanite Queens

Muktasari:

  • Tanzanite ilianza kupata kichapo ilipovaana na Simba Queens katika uwanja wake wa nyumbani Sheikh Amri Abeid mabao 2-1 kabla ya kunyukwa 6-0 na JKT Queens. Pia ilifungwa 2-1 na Yanga.

Arusha. Kocha wa ‘Tanzanite Queens’ ya Arusha, Abdallah Juma ametaja sababu za timu yake kuboronga katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza jana, Juma alisema matokeo ya kufungwa mechi tatu mfululizo yametokana na ugeni wa timu hiyo katika Ligi Kuu.

Tanzanite iliyopanda daraja msimu huu, haijavuna pointi katika mechi tatu ilizocheza hatua ambayo inaiweka timu hiyo kwenye mazingira magumu.

Tanzanite ilianza kupata kichapo ilipovaana na Simba Queens katika uwanja wake wa nyumbani Sheikh Amri Abeid mabao 2-1 kabla ya kunyukwa 6-0 na JKT Queens. Pia ilifungwa 2-1 na Yanga.

Hata hivyo, Juma alisema vipigo vimetosha kwa kuwa ameweka mkakati wa kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Mlandizi Queens.

“Tuko safarini kwenda Pwani kucheza na Mlandizi, tunaahidi kurudi Arusha na pointi tatu baada ya kuzikosa katika mechi zetu tatu,” alisema Juma.

Kocha huyo alisema njia pekee ya kufufua matumaini ya kubaki katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ni kushinda katika mechi zinazofuata