Waarabu wa Ulimwengu wapewa 'sumu' kuimaliza Simba

Muktasari:

 

  • JS Saoura imepangwa Kundi D, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi pamoja na timu za Simba, AS Vita ya Congo na Al Ahly ya Misri.

Kikosi cha JS Saoura cha Algeria pamoja na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam usiku wa leo Alhamisi tayari kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

JS Saoura iliyomsajili Ulimwengu ambaye ni Mtanzania na anaijua vizuri Simba watakayocheza nayo keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho ambacho kinakuja kikiwa na morali ya juu baada ya kupewa 'sumu' baada ya mazoezi yao ya mwisho na uongozi wa klabu ulioongozwa na Rais wa Klabu Mohamed Zerouatti.

Zerouatti amewaambia wafanye kila wanaloweza, warudi Algeria wakiwa na ushindi kwa sababu wanaimani na kikosi chao.

Msafara mzima wa JS Saoura unatarajiwa kutua Dar es Salaam kwa ndege maalumu ya kukodi.

Awali, Ulimwengu alikakaririwa akisema wanakuja kucheza na Simba wakiwa wamejiandaa na wanatarajia matokeo mazuri.