Try Again: Mo Dewji alinipigia simu!

Thursday October 11 2018

By Edo Kumwembe

Cape Verde: Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kutulia baada ya tukio la mwanachama mwenzao, Mohammed Dewji 'Mo' kutekwa na ameweka wazi kuwa alimpigia simu kabla ya tukio.
Try Again ni miongoni mwa wadau waliokwenda nchini Cape Verde kwa ajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa Stars.
Alisema, tukio hilo ni la kusikitisha na amewaomba Watanzania hususani wanachama wa Simba watulie.
"Jambo linalotakiwa kufanywa sasa ni kumwombea dua, ili mwenzetu awe salama huko alipo na jeshi la polisi linafuatilia kwa ukaribu suala hilo,"alisema Try Again.
Amefafanua kuwa, jana Jumatano, Mo alimpigia simu kuomba mawazo kwake na wakaongea kwa kipindi kirefu.
"Alikuwa na kikao cha bodi na kuna mambo aliomba nimshauri, lakini ndiyo hivyo tena," alifafanua.
Namna alivyowatuliza wachezaji wa Simba ambao wako na Taifa Stars nchini Cape Verde.

Advertisement