Tariq asaini Yanga

Muktasari:

Dirisha la usajili la Ligi kuu bara litafunguliwa Jumapili nat ayari timu mbalimbali zimeshaanza kuimarisha vikosi vyao ikiwemo Yanga ambayo imemsajili Tariq huku ikihusishwa pia kumtaka mshambuliaji wa Polisi Tanzania Ditram Nchimbi.

Mshambuliaji wa  zamani wa Biashara United,Tariq Seif Kiakala  amesaini mkataba wa  miaka miwili kuichezea  Yanga.

Usajili huo ni kama utawapa ahueni mashabiki wa Yanga ambao ni kama waikosa raha baada ya kuondoka kwa wachezaji wap  wawili Juma Balinya na  Sadney Urikhob ambao wamevunja mikataba na klabu hiyo.
 
Wachezaji hao waliachana na Yanga wiki hii baada ya kuomba kuvunja mikataba kwa kuchelewa kulipwa mishahara yao na klabu hiyo kuridhia wakidai nao walikuwa wanawapigia hesabu za kuwatema.

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla  amesema licha ya changamoto mbalimbali za kiuchumi wanaendelea kupambana kuisuka timu hiyo na kwamba Kiakala umetangulia tu.

"Tunafurahi kukamilisha usajili  wamchezaji huyu muhimu  ambaye kazi yake inajulikana kwa wanaofuatilia mpira hapa nchini wanajua Yanga tumechukua mchezaji wa namna gani," alisema Msolla.