TFF yakamilisha usaili uchaguzi Yanga

Saturday December 8 2018

By CHARITY JAMES

Dar es Salaam. Hatua za kuthibishwa kwa wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga imepit na majina yaliyopitishwa ni Jonas Tiboroha na Mbalaka Igangula wakati Erick Minga alienguliwa katika nafasi hiyo.
Zoezi la usaili lilifugwa saa sita mchana leo Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela.
Mchungahela amesema sababu za Erick Minga kuenguliwa katika nafasi hiyo ni mkanganyiko wa taarifa zake lakini pia aliwataja waliopita katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kuwa ni Pindu Luhayo Titus Asoro, Salam Chota.
"Upande wa Minga taarifa ambazo aliziwasilisha kwa njia ya maandishi ni tofauti na taarifa zilizokuwa katika kadi yake ya uanachama na alipohojiwa kuhusiana na hilo alishindwa kujieleza," alisema
"Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa ikiwaniwa na wagombea wanne lakini Yona Kavela ameenguliwa katika nafasi hiyo kutokana na kuchukua fomu mbili ya Mwenyekiti na Makamu kitu ambacho ni kinyume cha sheria," alisema.
Mchungahela aliwataja wajumbe waliopita katika kinyang'anyilo hicho kuwa ni Athanas Peter,  Ramadan Said, Salim Rupia, Dominic Francis, Shafii Amri, Benjamim Mwakasonde,  Christopher Kashililika, Ally Omary, Sylvestor Haule,  Arafat Haji, Frank Kalokole na Said Kambi.
"Wagombea, Hamad Ismail, Bernard Mabula, Leonard Marongo na Seko Kongo walishindwa kufika katika usaili hivyo wameejiengua wenyewe katika nafasi hiyo," alisema Mchungahela.

Advertisement