Staa Yanga aapa kuwafunga Zesco

Muktasari:

Nyota wa Yanga ameapa kuhakikisha wanaitoa ZESCO United  ili kupata  tiketi ya kuingia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dar es Salaam. Jumamosi  ya wiki hii Yanga, itakuwa na kazi ya kutetea nafasi ya kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ZESCO ya Zambia, ambapo nyota wa kikosi hicho Fei Toto amesema watahakikisha wapinzani wao hawatoki.
Yanga imeingia hatua ya pili baada ya kuwaengua Township Rollers kwenye mechi ya awali ambapo Uwanja wa Taifa,matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1, ugenini ikashinda bao 1-0.
Fei Toto amesema wanaamini wataitoa ZESCO  kwa sharti ya kuanza vyema nyumbani, kisha ugenini kupambania sare.
"Tunaiheshimu ZESCO, hivyo tunajua tutaingia uwanjani kupambana na timu inayohitaji kusonga mbele kwenye michuano hiyo na sisi tunahitaji kutinga hatua ya mabingwa"
"Utakuwa mchezo mgumu, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa hamasa kwani tunaliwakilisha taifa, naamini hatutawaangusha"amesema.