Salum Mayanga kocha mpya Mbao FC

Muktasari:

Hata hivyo, Mayanga ambaye hakutana kuweka wazi alisema, atafutwe baadaye kwani alikuwa kwenye kikao.

Kocha Salum Mayanga amesaini mkataba mpya na Klabu ya Mbao FC leo Alhamisi akichukua mikoba ya Ally Bushiri aliyevunjiwa mkataba.
Mayanga amesaini mkataba huo baada ya kuachia majukumu ya Ukurugenzi ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar ambayo aliichezea na kuifundisha katika vipindi tofauti.
Katibu Mkuu wa Mbao FC, Danniel Naila ameweka wazi kuwa majukumu ya mkataba wao na Mayanga ni kuibakisha Ligi Kuu Bara.
"Mkataba wake ni mpaka msimu wa ligi utakapoisha na malengo ni hayo. Upo uwezekano wa kuongezewa mpya pale atakapokuwa na matokeo mazuri katika mechi zake,"alisema Naila.
Hata hivyo, Mayanga ambaye hakutana kuweka wazi alisema, atafutwe baadaye kwani alikuwa kwenye kikao.