Salamba, Mlipili na Kichuya wanunua ndinga za maana!

Shiza ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akitumia usafiri wa pikipiki, aliingia uwanjani hapo akiwa na gari.

 

BY Thobias Sebastian

IN SUMMARY

  • Wachezaji ambao awali hawakuwa na ndinga yaani magari lakini katika mazoezi yao ya jana Jumatano waliyofanya kwenye Uwanja wa Boko Veterani, waliibuka kivingine.
  • Waaliingia na magari yao huku kila mtu aliyekuwa uwanjani hapo, alibaki anashangaa nao ni Shiza Kichuya, Yusuph Mlipili na Adam Salamba.

Advertisement

Dar es Salaam. Ukifika kwenye mazoezi ya Simba kwa sasa lazima utashangaa kwa sababu ni kama wachezaji wote wanamiliki ndinga tena za maana.

Wachezaji ambao awali hawakuwa na ndinga yaani magari lakini katika mazoezi yao ya jana Jumatano waliyofanya kwenye Uwanja wa Boko Veterani, waliibuka kivingine.

Waaliingia na magari yao huku kila mtu aliyekuwa uwanjani hapo, alibaki anashangaa nao ni Shiza Kichuya, Yusuph Mlipili na Adam Salamba.

Shiza ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akitumia usafiri wa pikipiki, aliingia uwanjani hapo akiwa na gari aina ya Crownn yenye rangi nyeusi, Salamba ambaye awali gari ilipata ajali, ametinga na Crown pia lakini ni rangi nyeupe wakati Mlipili aliingia na Chevrolet nyekundu.

Kitendo hicho, ni kama kiliamsha hisia za mashabiki waliofika kuangalia mazoezi hayo na stori za magari hayo zikatawala.

 

More From Mwanaspoti
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept