Ray awaonya Simba mapema

Saturday August 10 2019

 

By ELIYA SOLOMON

MSANII wa Bongo movie, Ray Kigosi amesema kwa namna alivyokitazama kikosi cha Yanga msimu huu wa 2019/20  mashabiki wa Simba wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia.
Kigosi alisema Yanga imeshusha vifaa vya maana ambavyo vinaweza kuifanya timu hiyo kuwa tishio Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Naiona ile Yanga ya kimataifa iliyokuwa ikisumbua,  hakuna wakututisha na uwezo wa Simba ni nguvu za soda,  hutokuwa kwetu vizuri msimu uliopita kuliwafanya waonekana bora, " alisema msanii huyo.
Kigosi alisema Yanga inanjaa ya makombe hivyo kila atakayekuwa anakuja mbele yao atakuwa akikiona  cha moto,  iwe kwenye Ligi hadi kombe la Azam ambalo ni maarufu kama FA.
"Tunakiwango cha kuchukua makombe yote ya ndani, kuanza kwetu kuwa sawa kunawafanya muda wote wawe na presha wapinzani wetu, " alisema.
Yanga wanakabiliwa na kibarua cha kuing'oa Township Rollers ya Botswana kwenye mchezo wa awali wa kuwania nafasi ya kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement