Priyanka akerwa na ubaguzi wa rangi

Thursday May 16 2019

 

Nyota wa filamu Priyanka Chopra ameeleza wazi kukerwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi wanavyokutana navyo watu weusi katika jamii iliyotawaliwa na watu weupe.
Nyota huyu wa Hollywood mwenye asili ya India amesema hata yeye aliwahi kukutana na ubaguzi huo akiwa anasoma jambo lililokuwa likimnyima raha.
Alisema alikuwa kwenye wakati mgumu pale alipokuwa akitengwa na wenzake kwa sababu ya rangi yake ya udhulungi na kuonekana kama mtu asiyefaa kwenye jamii.
“Ni jambo amabalo linaumiza sana nafahamu maumivu wanayopata wanaopitia kwenye hali hiyo kwa kuwa hata mimi nilipitia, tuna kila sababu ya kupaza sauti na kupinga vitendo hivi vya ubaguzi kuanzia ngazi ya familia yani mtoto akue akifahamu kwamba binadamu wote ni sawa,”

Advertisement