Pointi moja ya Simba yampa kiburi Mpalile

Friday November 8 2019

 

By Charity James

TANGU mwaka 2012 Prisons ilikuwa haijawahi kuambulia japo pointi moja mbele ya Simba katika mechi ya ugenini jijini Dar es Salaam, lakini jana ilifanikiwa na hilo limempa kiburi nahodha wa maafande hao akianiki kitu kinachowabeba msimu huu ikiwa timu haijaapoteza mechi yoyote.


Nahodha huyo Laurian Mpalile amesema mbinu na ubora wa kikosi chao ndio siri ya mafanikio ya wao kuto kuruhusu nyavu zao kutikiswa hadi sasa.


Mpalile amefunguka hayo baada ya kupata pointi moja ugenini dhidi ya Simba na kuweka wazi kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kuwazuia mabingwa watetezi washindwe kufurukuta.


Simba na Tanzania Prisons wamegawana pointi moja moja badaa ya dakika tisini kumalizika bila ya kufungana.


Alisema wanajivunia kuambulia pointi moja ugenini dhidi ya timu ambayo hawajawahi kuifunga wala kuambulia sare zaidi ya miaka tisa wakiwa ugenini.


"Tumeweza kutimiza lengo kwa asilimia 50 kwa kuambulia sare nia yetu ilikuwa ni kupata matokeo ugenini kocha alifanya kila mbinu ili tuwqeze kupata matokeo lakini wapinzani wetu pia walikuwa makini na kutufanya tuishindwe kuwafunga," alisema.

Advertisement


"Baada ya sare hiyo mipango yetu ni kuendeleza rekodi ya kuto kuruhusu nyavu zetu kutikishwa tumekutana na timu ngumu zaidi ya timu zote ambazo tumekutana nazo hadi sasa walijua kutudhibiti kila kona na kuvuruga mipango," alisema.

Rekodi Simba v Prisons 2012-2019

Nov 07, 2019
Simba 0-0 Prisons

2018-2019
Ago 22, 2018
Simba 1-0 Prisons
Mei 05, 2019
Prisons 0-1 Simba
2017-2018
Nov 18, 2017
Prisons 0-1 Simba            
Apr 16, 2018
Simba 2-0 Prisons
2016-2017
Nov 09, 2016
Prisons 2-1 Simba            
Feb 11, 2017
Simba 3-0 Prisons
2015-2016
Okt 21, 2015
Prisons 1-0 Simba            
Mar 13, 2016
Simba   1-0 Prisons
2014-2015
Ok 25, 2014
Prisons 1-1 Simba            
Feb 28, 2015
Simba 5-0 Prisons
2013-2014
Okt 12, 2013
Simba  1-0 Prisons
Mar 09, 2014
Prisons 0-0 Simba           
2012-2013
Sept 29, 2012
Simba  2-1 Prisons
Feb 20, 2013
Prisons 0-1 Simba            

Advertisement