VIDEO>Pawasa: Simba ikipoteza utakuwa 'msiba wa kitaifa'

Saturday March 16 2019

By Mwandishi Wetu

Simba inacheza na AS Vita leo saa 1:00 usiku Machi 16, 2019 na amesema kuwa kufungwa kwa Simba itakuwa si nhuzuni kwa wachezaji wa Simba au mashabiki wake, kila Mtanzania ataumizwa na matokeo ya Simba kufungwa.

Amesema kuna ushabiki unaingia miongoni mwa mashabiki wa pande zote mbili, lakini katika eneo la mchezo wa Simba na AS Vita na Simba kushinda itakuwa nafasi bora kwa soka ya Tanzania.

Pawasa amesema kushinda kwa Simba kutakuwa na faida kwamba Simba itaingia robo fainali na ikifanya vizuri zaidi itatengeneza mazingira ya kuongeza timu za Tanzania kati michuano ya klabu mwakani.

"Itakuwa faida kwa taifa na ukiangalia hamasa iliyopo kila mmoja ninaamini anataka Simba ivuke, ukiangalia pia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, kwenye vijiwe vya kahawa stori ni Simba kila mmoja anataka kuisapoti Simba ivuke."

Hata hivyo, Pawasa amesema kuwa pamoja na hayo kinachotakiwa ni kwa wachezaji kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kujua kuwa kila Mtanzania anataka kuona wanasonga mbele.

"Wachezaji wajitolee kwa asilimia 120, wajitoe, wacheze kwa umakini na zaidi ni kuanzia kipenga cha kwanza hadi dakika 90 za mchezo," alisema Pawasa alipokuwa akizungumza jana asubuhi na kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC.

 

 

Advertisement