Mashabiki Yanga mapema tu kuiunga timu yao

Muktasari:

Katika mchezo wa kwanza kwenye Ligi hii Yanga waliitoa Township Rollers baada ya kutoka sare 1-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa na ule wa marudiano Yanga wakiibuka na ushinid 0-1 nchini Botswana.

MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameanza kuiunga mkono timu yao mapema baada ya kujitokeza Makao Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Jangwani na Twiga wakienda kununua jezi pamoja na tiketi za mchezo dhidi ya Zesco United.
Mwanaspoti Online limeshuhudia idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga wakinunua jezi kwa wingi.
Wakati mashabiki hao wakiwa wananunua jezi shughuli zingine klabuni hapo zilikuwa zikiendelea kama kawaida.
Yanga itacheza na Zesco United mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika majira ya saa 10 jioni, mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa awali wa ligi ligi hiyo Yanga waliitoa Township Rollers baada ya kutoka sare 1-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa na ule wa marudiano Yanga wakiibuka na ushinidi 0-1 nchini Botswana.