Mambo ya harusi ya Tambwe ndo kama hivyo!

Saturday November 10 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Ndani ya ukumbi wa CCM Ilala Boma, mambo yamepamba moto katika sherehe ya mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe na mkewe Raiyan Mohammed.

Sherehe hiyo ni maalumu kwa ajili ya utoaji wa zawadi na pongezi kwa wawili hao iliyoandaliwa upande wa mwanamke.

Tayari wageni waalikwa wameshaanza kuingia wakiwa katika sare za aina tofauti rangi ya pinki, nyeusi na nyeupe.

Maharusi bado hawajaingia, lakini burudani ya muziki ikiendelea na watu wanacheza na kupumzika.

Huu ni mwendelezo wa matukio tofauti kwanza ilianza singo, ikaja ndoa na leo usiku wa zawadi.

Advertisement