MO atimiza wiki, bado kiza kinene

Muktasari:

  • Wakati Watanzania, Afrika Mashariki na sehemu mbalimbali duniani wakiendelea kufuatilia taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ leo Alhamisi limetimiza wiki moja kamili

TUKIO la kutekwa kwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘MO’ leo Alhamisi limetimiza wiki moja kamili, lakini kiza kizito kimezidi kutanda juu ya kupatikana kwake huku familia ikiahidi kuitisha mkutano mwingine wiki ijayo ili kuzungumza na watanzania.

MO, alitekwa alfajiri Alhamisi iliyopita eneo ya Hoteli ya Colosseum, jijini Dar es Salaam alipokwenda kufanya mazoezi kama desturi yake na mpaka sasa hakuna taarifa njema juu ya kupatikana kwake.

Msemaji wa familia ya bilionea huyo, Azim Dewji ameliambia Mwanaspoti kuwa tangu walipotangaza dau na namba za simu kwa wasamaria wema kutoa taarifa za kupatikana kwa MO bado hawajapata lolote.

Azim, japo hakutaka kufunguka zaidi alisema huenda wiki ijayo familia ikafanya mkutano mwingine kuzungumza na Watanzania, ila alisema kwa sasa anaombwa aachwe hadi atakapokutana na wanafamilia.

Soma zaidi>