MGOMBEA SALIM RUPIA: Usajili wa Yanga utainufaisha klabu

Wednesday January 9 2019

 

By Charity James

MGOMBEA wa Yanga katika nafasi ya ujumbe, Salim Rupia amesema endapo atapata nafasi ya kuwaongoza wanayanga katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kipaumbele chake kikubwa ni kufanya usajili mzuri ambao utakuwa na manufaa kwa klabu.

Hayo aliyafema Jana alipokuwa akinadi Sera zake na kuweka wazi kuwa atatumia uzoefu alionao kuhakikisha anaisaidia Yanga kufika mbali zaidi kimaendeleo.

Alisema endapo atachaguliwa anaingia kwa kuchaguliwa lakini hadi sasa yupo yanga kwa kuteuliwa na anaiongoza katika nafasi ya kamati ya mashindano.

Alisema kipindi chake cha mwaka na nusu atahakikisha anasajili wachezaji kwa kuwafanyia scauti na kuangalia nahitaji ya timu huku akiweka kipaumbele cha kusajili wachezaji kulingana na kipato cha klabu.

"Usajili utaangalia timu inamajukumu gani mbele na utafanyika kwa kushirikiana na benchi la ufundi sitaweza kuwa miongoni kwa viongozi ambao wanafanya usajili bila kuangalia nahitaji ya benchi la ufundi," alisema.

 

Advertisement