Lipuli yamuhamisha Novatus Lufunga

Wednesday December 6 2017

 

By DORIS MALIYAGA

KIKOSI cha Lipuli kimefanya jambo moja kwa Novatus Lufunga, imemuhamisha namba kutoka beki wa kati aliyokuwa anacheza na sasa ni kiungo.
Lipuli imefanya maamuzi hayo kutokana na aina ya wachezaji walionao katika nafasi ya beki ya kati ambako kuna Joseph Owino raia wa Uganda na Mghana Asante Kwasi.
 "Awali, Lufunga alikuwa na majeraha ya nyama za paja lakini sasa anaendelea vizuri. Kuhusu nafasi ya kucheza uwanjani ni kiungo kwa sababu ndiko ameonakana anafanya vizuri zaidi, pia kwenye beki ya kati kuna wengine kama Owino na Kwasi,"anasema kiongozi wa Lipuli.
Lufunga alisajiliwa na Lipuli mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba, hata hivyo kikosi hicho kinachofundishwa na makocha, Amri Said na Seleman Matola, kipo kwenye mpango wa  kusajili wachezaji sita kwenye dirisha dogo.