Leo ndio leo, Yanga ni mwendo wa vipensi tu

Muktasari:

Yanga inaingia uwanjani leo Jumamosi kukipiga na Zesco United mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo ambao mashabiki wa Yanga waliweka wazi vazi lao litakuwa ni pensi tu.

Ile siku ambayo uongozi wa Yanga uliweka wazi utakuwa ni mwenzo wa vipensi ndiyo leo Jumamosi ambapo watakuwa na mchezo dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Vipensi hivyo vinavalia katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya kwanza na hii ikiwa ni kumuenzi Kocha Mwinyi Zahera anayekinoa kikosi hicho.
Vipensi hivyo vimehamasishwa ndai ya klabu hiyo baada ya Zahera kuadhibiwa na TFF faini ya dola 500 ambayo ni zaidi ya Sh. 1mil kwa madai kiongozi huyo aliingia uwanjani katika mchezo wao wa ligi dhidi ya JKT Tanzania na vazi hilo jambo ambalo hakuwa nadhifu.
Hata hivyo, pamoja na mashabiki kuhamasisha hivyo, Zahera amesema, ataangalia hali ya hewa namna itakavyokuwa uwanjani hapo. Ikiwa ya joto yeye atavaa pensi kama kawaida yake na ikiwa ya baridi atavaa nguo zinzoendana na hali hiyo ambazo zitakuwa ndefu.
Hata hivyo, mchezo wa leo si wa Ligi Kuu na uko chini ya CAF itategemea na mipango yao.
Yanga imeingia kucheza hatua hiyo baada ya kuwang'oa Mbabane Swalow wa Botswana.