Kumbe Moyes kamkataa Pogba

MANCHESTER, ENGLAND. ALA kumbe. Kocha David Moyes alipiga chini nafasi ya kumrudisha Paul Pogba klabuni Manchester United wakati alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2013.

Moyes alitua Old Trafford kuchukua mikoba ya Sir Alex Ferguson wakati alipong’atuka, lakini alijikuta akidumu kwenye kikosi hicho kwa miezi minane tu kabla ya kupigwa kibuti.

Usajili wa hovyo kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huo wa 2013, ulimshuhudia Moyes akimsajili Marouane Fellaini na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye kufeli kwake.

Man United ilihitaji kumsajili Pogba kipindi hicho, lakini kiungo wa Kihispaniola, Cesc Fabregas alikuwa chaguo la kwanza la Moyes hivyo alimtaka makamu mwenyekiti mtendaji, Ed Woodward kukatiza likizo yake kwenye kukamilisha usajili wa staa huyo, ambaye kipindi hicho alikuwa Barcelona. Man United na Barcelona zilifikia makubaliano.

Lakini, dili lilishindwa kukamilika na miezi 12 baadaye, Fabregas alikwenda kujiunga na Chelsea na kubeba taji la Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza tu Stamford Bridge.

Hivyo, Moyes akawa amemkosa Fabregas na Pogba aliyemkataa. Pogba aliondoka Man United mwaka 2012 kwenda Juventus baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi chini ya Ferguson, lakini miaka minne baadaye, Man United ikinolewa na Jose Mourinho, staa huyo wa Ufaransa alirudi kujiunga na mabingwa hao mara 20 wa England kwa ada ya Pauni 89 milioni.

Kabla ya Mourinho kutua OT.