Kumbe Kagera Sugar walijua wanachapa mtu bwana!

Sunday September 16 2018

 

By Berdina Nyakeke

Musoma. Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema, waliifuata Biashara United nyumbani kwao wakiamini watawafunga lakini wamepata suluhu ya ugenini kwao poa tu.

Maxime aliyeanza na kumaliza maisha yake ya kucheza soka Mtibwa Sugar na baadaye akawa kocha kabla ya kuachana nao na kujiunga na Kagera.

Amesema: “Tulijipanga kuona tunaifunga Biashara, lakini kwa bahati mbaya tukaambulia pointi moja ambayo hata hivyo, tunashukuru kuipata.”

Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars amesema, bado timu hiyo ina matumaini ya kufanya vizuri katika michezo yake bila kujali anakuwa ugenini au nyumbani.

"Niseme wazi kuwa bado tuna imani ya kufanya vizuri zaidi kwenye ligi, mechi ndiyo kwanza zimeanza,"alisisitiza.

Advertisement