Kumbe Bruno Fernandes tatizo mkwanja tu kutua Man United

KUMBE kinachomchelewesha Kiungo wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes, 25, kutua Manchester United wakati huu wa dirisha dogo la usajili ni pesa tu.

Ishu iko hivi;- Man United imeshamalizana kila kitu na Fernandes mwenyewe, lakini shida inakuja kwenye pesa ambayo Sporting Lisbon inaitaka ili kumuachia kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno.

Sporting inataka Pauni 68 milioni, lakini Man United haiko tayari kulipa pesa hiyo kwa sababu inaamini ni nyingi sana kulinganisha na thamani halisi ya Fernandes.

Man United imeiambia wazi Sporting kuwa dili hilo litakufa kama haitapunguza bei na tayari miamba hiyo ya Old Trafford imeanza kuangalia viungo wengine ikiwa itamkosa Fernandes.

Kama Manchester United itakomsa kiungo huyo, hii itakuwa ni mara ya pili kwa kuwa awali ilimtaka katika dirisha lililopita la majira ya joto. Katika dirisha hilo ilifika hatua hata Fernandes kuaga kwa wachezaji wenzake.