Koffi Olomide ahukumiwa miaka miwili kwa ubakaji

Muktasari:

  • Pia Mahakama hiyo ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawasawa kwa kosa la kuwasaidia wanawake watatu kuingia nchini ufaransa kinyume na sheria.

Mwanamuziki wa Congo, Koffi Olomide  amehukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili baada ya mahakama ya Nanterere nchini Ufaransa kumtia hatiani kwa mashtaka ya ubakaji wa mnenguaji wake alipokuwa na miaka 15.
Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu, huku Koffi Olimide akiwa hayupo mahakamani hapo.
Hata hivyo, Olimide mwenye mwenye miaka 62 aliamriwa alipe Euro 5,000 ikiwa ni fidia  kutokana na madhara aliyomsababishia mnenguaji huyo.
Pia Mahakama hiyo ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawasawa kwa kosa la kuwasaidia wanawake watatu kuingia nchini ufaransa kinyume na sheria.
Wakili wa mwanamuziki huyo, Emmanuel Marsigny amepongeza uamuzi huo wa mahakama na kuutaja kuwa ni ushindi kwani baada ya hukumu kutolewa mteja wake atakuwa ameupuka waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake.
Hata hivyo, waendelesha mashtaka walikuwa wakishinikiza ahukumiwe miaka 7 gerezani lakini mahakama imetupilia mbali mashataka ya unyanyasaji na madai ya utekaji nyara yaliyokuwa yakimkabiri.
Awali, wanenguaji wanne waliokuwa aliokuwa akifanya nao kazi waliiambia mahakama kwamba mwanamuziki huyo, aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006. Walieleza kuwa unyanyasaji huo ulifanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ufaransa.
Pia wanawake hao walieleza kwamba walizuiwa katika nyumba moja nje ya mji wa Paris na walifanikiwa kutoroka usiku wa Juni 2006, lakini hawakurudi DR Congo kutokana na kuogopa kutafutwa na kulipiziwa kisasi.
Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, amejikuta matatani mara kadhaa:
•    2018: Zambia iliagiza akamatwe baada ya kutuhumiwa kumshambulia mpiga picha
•    2016: Alikamatwa na kutimuliwa baada ya kumshambulia mojawapo ya wanenguaji wake Kenya
•    2012: Alishtakiwa DR Congo kwa kumshambulia produza wake na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu ambacho angefungwa iwapo angefanya kosa jingine
•    2008: Alishutumiwa kumpiga teke mpigapicha katika kituo cha Televisheni DR Congo RTGA na kuivunja kamera yake katika tamasha, lakini baadaye jambo hilo walilimaliza.