Kocha, Aussems, achanganye, karata, vizuri, simba, yaichapa, JS, Saoura

Muktasari:

Simba yapewa dawa ya kuwamaliza wapinzani wao JS Saoura hatua ya kwanza ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

TIMU ya JS Saoura inaweza kugonga mwamba kuisoma Simba kwenye Kombe la Mapinduzi huku wakiwa na baadhi ya majina wanayotembea nayo akiwemo Erasto Nyoni aliyeumia na hivyo hataweza kucheza.
Simba inawakalibisha JS Saoura Uwanja wa Taifa Jumamosi hii, hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tayari wapinzani wao wapo Zanzibar na wanajua hilo, hivyo imeelezwa wanaweza wakapindua ndege angani na hivyo malengo ya kuwasoma yasitimie.
Majina yanayotajwa ni hatari kwao kwenye kikosi cha Simba, halikosekani la Meddie Kagere, John Bocco, Nyoni, Cletus Chama na wengine.
Wataalamu wa soka nchini, wamemshauri Kocha Patrick Aussems, kubadilisha gia angani, kimbinu, upangaji wa wachezaji wa nani aanze na nani aingie kipindi cha pili.
Kocha wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibaden 'King Mputa' amesema Aussems anaweza akatumia mfumo tofauti na waliousoma wapinzani wake kwenye Kombe la Mapinduzi.
"Namwamini Kocha Aussems kwa mbinu alifanya hivyo dhidi ya Mbabane Swallows walitegemea kwao angejilinda akaja na mbinu ya kushambulia ambayo iliwatoa mchezoni,"alisema Kibadeni.
"Kuumia kwa Nyoni itawafanya wajiamini kwa Simba itawapa nguvu ya kupambana zaidi, hilo litawafanya washinde mchezo, lakini pia anaweza akawatumia wachezaji ambao hawakutarajiwa wakabakia na majina yao mfukoni."
Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ulimboka Mwakingwe amesema bado kuna mbinu za kuwafanya Simba washinde dhidi ya JS Saoura, akidai wachezaji wanatakiwa kuhamasishana na kuweka dhamira ya pamoja.
"Zamani tulikuwa tunajiwekea malengo makabisa kwamba lazima tutoke na ushindi na ilikuwa hivyo, hivyo wachezaji wasisubiri maelekezo ya kocha ndipo waanze kuamsha akili zao, kila mmoja awe tayari kwa mchezo na watashinda mabao mengi tu,"anasema.