Klabu EPL kukodisha baiskeli

LONDON, ENGLAND. KLABU za Ligi Kuu, England zmedhamiria kuja na mfumo mpya wa kukodisha baiskeli ambazo zitatumiwa na mashabiki ili kuingilia uwanjani kama njia mojawapo ya kupambana na janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Serikali ya England ilikuwa inataka kuhuruhusu idadi ndogo ya mashabiki iingie viwanjani kwenye michezo za wiki hii, lakini mchakato huo ulisitishwa baada ya maambukizi kuongeza nchini humo.

Taarifa zilizotolewa na tovuti ya The Sun zinaeleza kuwa klabu za Ligi Kuu ya England zimekuwa kwenye mpango wa kuwasilisha mapendekezo lukuki kwa serikali ya nchini humo ili kuishawishi iruhusu mashabiki waingie viwanjani.

Kufuatia hatua hiyo klabu hizo zilipendekeza kuwepo kwa mfumo wa kukodisha baiskeli na kufunguliwa maduka mengi ya kuuuzia baiskeli ambazo ndio zitatumika kama usafiri wa mashabiki kuendea viwanjani ili kuondoa msongamano kwenye usafiri wa umma.

Mapendekezo mengine ni kuongeza ukubwa wa maegesho ya magari, na kuzishawishi kampuni za treni za abiria kuongeza treni.