Beki JKT Tanzania atoa siri ya kipigo

Muktasari:

JKT Tanzania ipo nafasi ya nane baada ya kucheza michezo 11, imeshinda minne, imetoka sare mitatu na imefungwa mechi nne na kufikisha pointi 15.


BEKI  wa JKT Tanzania, Adeyum Ahmed amefunguka sababu za wao kupoteza mchezo wao dhidi ya Yanga kuwa ni kuingia kwa uoga kwenye mchezo huo na kuzinduka muda ukiwa umeshaisha.

JKT Tanzania jana ilikubali kipigo cha bao 3-2 ugenini dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo alisema dakika 45 za kipindi cha kwanza ndio zilizowaponza na kujikuta wanapoteza umakini kitu ambacho ndio kilichowaghalimu.

"Yanga hawakuwa wazuri sana sisi wenyewe tulijipoteza kwa jkucheza bila kujiamini dakika 45 za kipindi cha pili tulirudi mchezoni na kuonyesha kile tulichoambiwa na mwalimu kwa kiasi kikubwa tulifanikiwa na ndio maana hatukutaka waingie kabisa eneo letu la hatali," alisema.

"Umakini mdogo wa safu yetu ya ushambuliaji nao pia ulitughalimu kwani walishindwa kutumia mapungufu ya safu ya ulinzi ya Yanga ambayo ilikuwa inapoteana na kujikuta wanaishia kutoa pasi mbovu ambazo zilikuwa zinaishia miguuni mwa mabeki," alisema.