Kipigo cha Liverpool; Ruud Gullit amkaanga Van Dijk

Muktasari:

Van Dijk alifanya uzembe ulimpa nafasi Saul Niguez kufunga bao katika mchezo huo ambao Liverpool ilifungwa bao 1-0.

London, England. Ruud Gullit amemponda beki wa Liverpool Vilgir van Dijk kwa uzembe aliofanya katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

Alisema Van Dijk alifanya uzembe ulimpa nafasi Saul Niguez kufunga bao katika mchezo huo ambao Liverpool ilifungwa bao 1-0.

Kauli kama hiyo pia imetolewa nahodha wa zamani Ufaransa Marcel Desailly ambaye kama Gullt walikuwa wachambuzi  juzi usiku.

Ndani ya dakika tatu van Dijk alifanya makosa mawili, alitaka kujifunga aliposhindwa kuokoa mpira wa krosi kabla ya Niguez kufunga kutokana na uzembe wake.

“Van Dijk leo (jana) usiku umekuwa mgumu kwake, niliomuona akifanya makosa mpira wa kwanza tu aliotoa kona wakati hakuwa na ulazima,”alisema Gullit ambaye ni Mholanzi kama beki huyo wa kati.

Desailly alisema licha ya ubora wake akiwa kwenye uwanja wa Anfield, lakini mchezaji mzuri anaweza kufanya makosa kwa kuwa haya ni mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.