King Kikii, Nguza Viking kupanda jukwaa moja

Wednesday December 5 2018

 

By Rhobi Chacha

Wimbo mpya kuwakutanisha King Kikii, Nguza Viking jukwaa moja Wanamuziki King Kikii na Nguza Viking wanatarajia kufanya uzinduzi wa muunganiko wao utakaofahamika kwa jina la 'Bakolo Mbonda' (Wakubwa wa Ngoma).
Uzinduzi huo utafanyika kuanzia Desemba 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Police Officers Mess uliopo Masaki na kila Ijumaa watakuwa wanapiga hapo.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Mratibu wa onyesho hilo, Khamisi Dacota amesema,muunganiko wao ni maalumu kwa ajili ya kukata kiu za mashabiki wa muziki huo hasa wale wa zamani (watu wazima) ambao walikuwa wakihitaji burudani hiyo irudi baada ya kimya cha muda mrefu.
Dacota amesema ikumbukwe awali ulikuwa ukifanyika Usiku wa Bakulutu ikiwa ni muunganiko wa wasanii Nguza Viking, Kikii na marehemu Ndala Kasheba na ulifunjika baada Nguza kupata matatizo na Ndala Kasheba kufariki dunia.

Advertisement