Karia: Ukiwa mzalendo hukati tamaa mapema

Wednesday June 26 2019

 

By Khatimu Naheka

Cairo, Misri. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallece Karia amesema anashangaa mashabiki wa soka wakikata tamaa baada ya Taifa Stars kupoteza mechi moja.

Karia amesema shabiki wa kweli na mzalendo hawezi kukata tamaa wala kuanza kutoa lugha kali wakati timu bado ipo katika mashindano.

Aidha Karia amesema katika mechi mbili zilizosalia wachezaji wamemuahidi kufanya vyema kuipigania nchi yao

Aidha Rais huyo alisema bado ana imani na makocha wa timu hiyo na kwamba matokeo ambayo wameyapata ni sehemu ya mchezo wa soka.

Rais huyo ambaye yuko na Stars hapa jijini Cairo alisema wamekuwa akizungumza na wachezaji ambao nao bado wako katika morali ya kupambana.

Jana baada ya mazoezi Karia alitumia dakika 15 kuongea faragha na wachezaji hao bila uwepo wa makocha katika mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Petrosport.

Advertisement

Advertisement