Kakolanya: Sina hofu na Manula

Muktasari:

Kakolanya anaenda kukutana na Manula ambaye amekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambayo ipo Misri kwaajili ya fainali za mataifa ya Afrika.

KIPA  mpya wa  Simba, Benno Kakolanya, amesema  anaamini kiwango chake hivyo hana presha ya kuwania namba mbele ya kipa namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula.
Beno amesaini Simba mkataba wa miaka miwili ambapo atakuwa kwenye upinzani wa namba na Manula ambaye pia ni kipa namba moja wa Taifa Stars.
Wawili hao wamewahi kuichezea Stars kwa pamoja ingawa Kakolanya alikuwa akikalishwa benchi na Manula.
Kakolanya anasema hajajiunga na Simba kwa lengo la kuwa mbadala wa Manula au Deogratius Munishi 'Dida', bali ni kupambana kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hicho.
“Naheshimu uwezo wa Manula na Dida lakini kwa nafasi yangu nitaonyesha nilichonacho, sina presha wala nini na nimekuwa nikisikia mengi kuwa huu ndio mwisho wangu nadhani watu hawajui maisha ya mpira yalivyo.
“Nimekuwa na maisha mazuri Yanga na yenye furaha, nadhani umefika muda wa kuangalia mbele ili kukabiliana na maisha mapya,” alisema Kakolanya.
Kipa huyo, anasema atatumia uwezo wake kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho eneo la makipa ambalo limeanza kutajwa msimu ujao litakuwa na ushindani wa aina yake.
“Nitashirikiana na Manula pamoja na Dida, naamini tutafanya kazi nzuri msimu ujao,” anasema