James Rodriguez ahitajika Madrid

Muktasari:

  • Florentino Perez amesema ikiwa klabu hiyo inahitaji kuendelea kuwa naye iketi mezani na kufanya makubaliano mapya.

Madrid, Hispania. Klabu ya Real Madrid imesema kuwa inakusudia kumrudisha mshambuliaji wake raia wa Colombia, James Rodriguez.

Katika taarifa yake Madrid imesema inamuhitaji mshambuliaji huyo aliyekua akikipiga kwa mkopo Bayern Munich ya Ujerumani, ambako alikuwa na mkataba hadi Juni 30, 2019.

Rais wa Madrid, Florentino Perez amesema ikiwa klabu hiyo inahitaji kuendelea kuwa naye iketi mezani na kufanya makubaliano mapya.

Madrid imebainisha kuwa mshambualiji huyo aliuzwa kwa mkopo kwa sababu alikua haivi na Kocaha Zinedine Zidane, hivyo waliona sio busara aendee kukaa klabuni hapo.

Imedokezwa kuwa uamuzi wa klabu hiyo umeshinikzwa na ujio wa Kocha mpya, Julen Lopetegui, ambaye anaukubali uwezo wa  James.

Mshambuliaji huyo mkataba wake na Madrid unatarajiwa kufikia tamati Juni 30, 2021, alikua na mwanzo mzuri Estadio Santiago Bernabeu kabla ya kutofautina na Zidane.

James alitua Madrid mwaka 2014 baada ya kung’ara vilivyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huo nchini Brazil.

Alipotua Madrid na kuwa chini ya Kocha Carlo Ancelotti, James oalifunga mabao 17 na kupika 18 katika mechi 46, lakini hakupata nafasi kwa Rafa Benitez na baadaye Zidane.