Ishu ya Sven, Ajib ni hii

Sunday May 31 2020

 

By MWANDISHI WETU

KATIKA kuhakikisha nidhamu inakuwepo ndani ya timu, Kocha Sven Vanderbroeck amethibitisha kumtimua mshambuliaji wake Ibrahimu Ajibu kwa kosa la kuchelewa kujiunga na wenzake na atamrejesha kambini keshokutwa  Jumatatu.

Sven alifafanua kuhusu sakata hilo kwamba;, “Ajibu alichelewa, nikiwa kama kocha nikawajibika kumrudisha nyumbani ikiwa ni sehemu ya kumuadhibu. Nadhani anaweza kurejea kikosini Jumatatu.”

Katika mazoezi ya jana, Vandenbroeck alionekana kuendelea kufanyia kazi utimamu wa miili ya wachezaji wake kwa kufanya mazoezi mbalimbali ambayo  yalionyesha wazi  kuwajenga wachezaji wake.

Katika mazoezi ya siku mbili za kwanza wachezaji hao wa Simba walifanya mazoezi mara mbili na kila siku moja walifanya mazoezi ya nguvu kwa saa tatu.

Advertisement