Haruna aanza na bao KMC

Friday January 17 2020

 Haruna aanza na bao KMC-Kocha Haerimana Haruna-Mtibwa uwanja wa Uhuru- Dar es Salaam- Jackson Mayanja-

 

By Mwandishi Wetu

Kocha Haerimana Haruna ameanza kazi rasmi leo Ijumaa akiwa na timu yake mpya ya KMC inayopambana na Mtibwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
KMC imemchukua kocha huyo kutoka Lipuli ya Iringa ambayo ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, huku timu yake mpya ikiwa nafasi ya 17.
Haruna alijiunga na Lipuli mwanzoni mwa msimu huu akichukua nafasi ya Selemen Matola, lakini akadumu ndani ya timu hiyo kwa miezi sita tu kabla ya kuchukuliwa na KMC.
Kocha huyo ameonekanaa amekaa benchi muda mwingi wa mchezo katika kipindi cha kwanza  huku msaidizi wake Hamad Ally, wakisimama kutoa maelekezo kwa wachezaji.
Mpaka sasa KMC inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Sadalah Kipangile dakika ya 18.

Advertisement