Gaucho: Inaanza Stars kisha Kili Queens

Muktasari:

Michuano ya Cecafa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam ambapo timu nane zitashiriki.

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Heroes' Mwanahamisi Omary 'Gaucho' amesema, anajua mashabiki wa soka la Tanzania wanataka furaha jambo ambalo wamejiandaa kuwapa.
Lakini, kabla ya wao anaimani furaha hiyo itaanzishwa na kaka zao wa Taifa Stars ambao, leo wanakipiga na Equatorial Guinea mechi ya kwanza hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021.
"Mashabiki wetu tunawajua tutawatendea haki kikubwa watupe ushirikiano tu na katika kuwahakikishia hilo, kaka zetu wataanza na Equatorial Guinea na sisi tutamaliza kwenye cecafa ni raha juu ya raha," alisema Gaucho.
Michuano ya Cecafa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam ambapo timu nane zitashiriki.
Tanzania Bara imepangwa Kundi A, pamoja na Zanzibar, Burundi na Sudan Kusin, Kundi B, lina Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibout.