Eti joto limeing'oa Singida United michuano ya SportPesa!

Muktasari:

Singida imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano ya Kombe la  SportPesa baada ya kuchapwa bao 1-0  na Bandari, bao la washing lilifungwa na  William Wadri kwa penalti baada ya Boniface Maganga wa Singida United kushika mpira eneo la hatari.

Dar es Salaam. Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bandari ya Kenya kimemvuruga kocha wa Singida United, Dragan Popadic ambaye amewatupia lawama waamuzi huku akilalamika kuwekwa katika chumba chenye joto kali.
Popadic alisema Kama waamuzi wataendelea kuchezesha hivyo basi soka la Afrika halitaendelea.
Singida imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano ya Kombe la  SportPesa baada ya kuchapwa bao 1-0  na Bandari, bao la washing lilifungwa na  William Wadri kwa penalti baada ya Boniface Maganga wa Singida United kushika mpira eneo la hatari.
Baada ya mchezo huo Popadic aliyeoonekana kuwa na hasira alisema  hakupendezwa na maamuzi ya waamuzi kwani yaliinyonga timu yake
"Hatukuwa  vizuri  kwani tulishindwa kutengeneza nafasi na kufunga.
 "Waamuzi waliharibu Sana  mchezo,kwani  Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine Afrika Kama waamuzi wanakuwa juu ya soka ni hatari.
" Pia tumekuja Dar es Salaam," alisema kocha huyo.
Alisema  watarejea kwenye ligi Ili kuhakikisha wanafanya vizuri  na baada ya Ligi kumalizika ataiunda upya timu yake.