Duu! Kilichomkuta Sarpong balaa

Friday October 09 2020
sapong pic

KUMBE kabla ya mechi Mtibwa Sugar na Yanga, Dickson Job aliwaambia washikaji zake kikosini kuwa atakula sahani moja na Michael Sarpong ingawa anasemekana kuna baadhi walimbishia na ndio chanzo cha yeye kufanya sifa.

Za chinichini ni kuwa Job alijipa muda wa kumsoma mshambuliaji huyo anayetegemewa kwenye kikosi hicho cha Yanga.

Licha ya udogo wa umbo lake, ahadi yake ilithibitika kwenye mchezo huo ambao hata hivyo Mtibwa Sugar walipoteza wakiwa nyumbani  kwa bao 1-0 ambalo walifungwa na Lamine Moro.

Sarpong hakutembea mbele yake kwani alikuwa akimkaba kwa nguvu kwa kuiga mbinu za swahiba yake, Kelvin Yondan.

Aliwahi kukakariwa akisema, "Kelvin ni kaka yangu nimekuwa nikijifunza vingi kutoka kwake."

Staa huyo wa Mtibwa Sugar ni sehemu ya kikosi cha Taifa Stars ambacho kinajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi.

Advertisement

..

Advertisement