Duh! Chirwa atua Zenji na kuomba jezi

Muktasari:

Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Samuel Lukumay ametua na Chirwa Zanzibar leo hii pamoja na kocha wa timu hiyo, Mzambia  George Lwandamina.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Obrey Chirwa ametua, Zanzibar lakini kabla ya kabla ya kupanda boti aliwashtua viongozi wa klabu hiyo akipowaambia yuko sawa na kama akipewa jezi sio atacheza bali hata kufunga atafanya hivyo.

Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Samuel Lukumay ambaye ndiye aliyetua na Chirwa Zanzibar leo hii pamoja na kocha wa timu hiyo, Mzambia  George Lwandamina.

Lakini wakati wako njiani mshambuliaji huyo amemtamkia kuwa hata akipewa jezi sio tu yuko tayari kucheza bali hata kupiga bao katika mechi yoyote atakayopewa nafasi.

Lukumay ambaye amedumu katika kamati hiyo kwa muda mrefu anasema, Chirwa amekanusha mbele yao kwamba, kukaa kwake Zambia kwa kipindi kirefu hakutokani na mgomo.

Kigogo huyo anasema, kauli ya Chirwa kuwa yuko tayari kuichezea timu hiyo hata sasa iliwashtua na wao wamewaachia makocha katika kuangalia ni lini mshambuliaji huyo anaweza kuanza kucheza.

Chirwa amesema amerejea kutumikia mkataba wake ambapo juzi alikutana na uongozi wa Yanga ambao walimwambia madai yake mbalimbali yatashughulikiwa kwa pamoja.

"Chirwa ni kweli nimefika naye huku Zanzibar yuko sawa na ameniambia kwamba sio kweli kama aligoma eti anadai na amesema anajua mambo ya klabu ndiyo maana amekuwa mvumilivu lakini alichotushtua ni pale aliposema yuko tayari wakati wowote sio tu kucheza hata kufunga,"anasema Lukumay.

"Tumefurahi kusikia hivyo lakini hayo yatakuwa ni maamuzi ya makocha kama viongozi hatupango timu na amewaomba Wanayanga kuachana na hizo taarifa kwamba aligoma anachotaka ni kuutumikia mkataba wake."