Dida afanya maamuzi magumu Yanga

Muktasari:

Wakati wanaingia uwanjani kwa ajili ya kiputwe hicho, mashabiki wa Yanga walimwita Dida na kumshangilia na yeye ikabidi awape salamu kwa kuwanyooshea mikono juu

Dar es Salaam. Mlinda mlango wa Simba, Deogratius Munishi Dida' ilimbidi afanye maamuzi magumu katika mchezo wao na Yanga uliopigwa leo Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Dida ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba katika mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Wakati wanaingia uwanjani kwa ajili ya kiputwe hicho, mashabiki wa Yanga walimwita Dida na kumshangilia na yeye ikabidi awape salamu kwa kuwanyooshea mikono juu, jambo ambalo ni gumu kufanywa na wachezaji wakati wapinzani hao wanapokutana.

Hii ni kutokana na ushindani uliopo Kwa timu hizo kongwe na pinzani nchini Tanzania. Awali, Dida aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio miaka ya nyuma kabla ya kurudi na kujiunga na Simba kwa mara nyingine.