DRFA kufanya mkutano mkuu wa mwaka

Friday November 29 2019

 DRFA- kufanya -mkutano- mkuu - mwaka-CHAMA- Soka -Mkoa-Dar es Salaam-mkutano-michezo blog-mwanasport-MwanaspotiSoka-MwanaspotiGazeti-

 

By Olipa Assa

CHAMA cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kinatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka siku ya Jumapili, Desemba Mosi, Dar es Salaam huku ajenda 10 zikitarajia kujadiliwa.

Baadhi ya ajenda kubwa zitakazojadiliwa kwenye mkutano ni uwasilishwaji na kujadili mpango mkakati wa miaka minne, kuthibitisha taarifa za utekelezaji wa kamati ya utendaji, kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliopita.

Ajenda nyingine ni kuthibitisha chombo  cha ukaguzi, kuthibitisha bajeti ya mwaka unaofuata na mengine mengi kwa ajili ya maendeleo ya DRFA.

Afisa Habari wa DRFA, Karim Boimanda amesema mkutano huo utaanza saa 2:00 asubuhi Uwanja wa Taifa, ili kuwapa nafasi wadau kujitokeza kwa wingi.

"Ni mkutano muhimu kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu cha mkoa, naamini wadau wa soka watajitokeza kwa wingi,"amesema.

Advertisement