Chirwa aliwachanganyia rangi Azam FC

Muktasari:

Mchezaji akiwa ameonyesha kiwango kizuri anakuwa na uhakika na biashara yake ya soka kwenye kipindi cha usajili, hicho ndicho anachokifanya Obrey Chirwa kuwadengulia Azam FC ambao amemaliza nao msimu.

OBREY Chirwa aliwakaushia Azam FC baada ya uwepo wa kutakiwa na Yanga, hivyo uongozi huo umeamua kusalenda na kwamba hawawezani na staa huyo licha ya kukiri kwamba alikuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi chao.
Chirwa alijiunga na Azam FC kupitia usajili wa dirisha dogo, akitokea Nogoom El Mostakbal Football Club ya nchini Misri, akipokewa mikononi mwa kocha Hans Pluijm ambaye baadae alitimuliwa baada ya timu kupata matokeo mabovu.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' amekiri kwamba baada ya kushindwa na na Chirwa, wameamua kumpa mkono wa kwa heri ili akaanze maisha sehemu nyingine.
Anasema wamekaa chini na Chirwa mara nyingi, lakini mchezaji huyo ni kama alikuwa anawafungia vioo akitaka wasubiri mpaka ligi imalizike na mwisho nwa siku wakaona hasomeki.
"Ukweli ni kwamba tulimhitaji mchezaji huyo kuwa miongoni mwa wachezaji ambao tutakuwa nao msimu ujao, lakini hatuna namna inabidi tumwache afanye kile anachokitaka"anasema Popat.
Azam wameachana na wachezaji nane ambao ni Ramadhan Singano, Joseph Kimwaga, Chirwa, Enock Atta, Twafazwa Kutinyu, Steven Kingu na Danny Lyanga