Buku 7 tu unamcheki Makambo, Okwi

Friday September 14 2018

 

By THOMAS NG’ITU

KAMA ni mashabiki wa Yanga au Simba walikuwa wakifurahia juu ya taarifa gemu la watani limeahirishwa, pole yao kwani mabosi wanaosimamia soka nchini (TFF) wamesisitiza gemu lipo palepale, tarehe ileile.

Juzi zilienea taarifa kuwa, mchezo huo ungesogezwa mbele kutoka Septemba 30 hadi tarehe nyingine, ili kupisha kambi ya Taifa Stars itakayojiandaa na mechi zao za Afcon 2019 dhidi ya Cape Verde. Hata hivyo jana Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema gemu lipo kama kawaida na kwamba kiingilio cha chini Uwanja wa Taifa siku hiyo kitakuwa buku 7 tu (Sh 7,000) na cha juu buku 30.

“Mchezo utapigwa kama kawaida siku uliopangwa utakuwa mchezo wa kuvutia na usalama wa kutosha,” alisema.

Ndimbo alisema tiketi zitaanza kuuzwa Septemba 20 na kwamba VIP A itakuwa Sh 30,000 huku VIP B itakuwa Sh 20,000 na majukwaa mengi yatakuwa Sh 7,000 tu.

Hilo litakuwa pambano la 101 kwa timu hizo katika Ligi Kuu tangu mwaka 1965 huku Yanga ikiwa na rekodi ya kushinda mechi 36 dhidi ya 30 za watani wao, huku michezo 34 ikimalizika kwa sare.

Advertisement